Sunday, September 18, 2011

Mtihani wa magonjwa wa zinaa katika DUC

Ijumaa ijayo huduma ya afya ya wanafunzi na Phi Lambda Psi (kikundi cha afya ya wanawake na akina mama) zitafadhili mkasa ya kupima kwa magonjwa wa zinaa.  Mkasa huu utakuwa bure kwa wanafunzi wote ambao wanahudhuria Wash U.  Wataweza kupimwa kwa kaswende na HIV kwa damu; kisonono na klamidia kwa mtihani wa mkojo; na HIV kwa mtihani wa usufi.  Huduma ya afya ya wanafunzi itawapa wanafunzi stikas, kondom kungoja salama!



Msamiati:

-fadhili: fund, sponsor
mkasa: event
-pima: test, assess
magonjwa wa zinaa: STD
-hudhuria: Wash U
kaswende: syphilis
damu: blood
kisonono: gonorrhea
mkojo: urine
usufi: swab


Carrie

Wednesday, September 14, 2011

Maisha yangu (Pat)

Watu wengi hutumia ratiba na mipango ili walikuandaa shughuli na matukio katika maisha zao. Maisha yangu ni tofauti sana. Mimi ninaandika ma wazo mara chache. Kila katika kichwa yangu. Ni nzuri kwa sababu ninakumbuka vizuri sana. Ni mbaya kwa sababu ikiwa ninasahau vitu halafu sitafanya vitu. Sasa ninajaribu kuandika "kufanya orodha" ili nitakumbuka wapi na wakati ninahitaji kwenda mahali na pamoja na nini. 

Mwaka huu, nitajaribu kuwa mtu bora. Sasa, mimi ni rais ya shirika inaitwa "Learning to Live." Na mimi ni mfanyakazi ambaye ana mawili. Na pia ninafanya kazi na shiriki (kujitolea)!

Maneno
ratiba - schedule
kuandaa - organize
matukio - events
mipango - plans
"kufanya orodha" - "to do lists"
mahali - places

Jiografia, Upande na Lugha

Tumesoma kuhusu athari za mazingira na jiografia kwa utamaduni, uchumi, na biashara. Kuna athari nyingi kwa lugha pia. Mara kwa mara jiografia ama inawezesha mazungumzo na biashara kati ya jamii kutoka sehemu tofauti za bara, au inazuia mazungumzo haya. Mweza kuona athari hii katika Kaskazini ya Afrika, na jangwa la Sahara, na katika Katikati ya bara, na msitu mkuu wa DRC.

Na pia, kuna athari nyingi zinazokuja kutoka mazingira na jiografia lakini zinazoitwa "Spatial Relations." Hii ni wazo kwamba watu wagawanya sehemu karibu na wao kwa mujibu wa mawazo yao kuhusu watu na ardhi. Kwa mfano, jamii nyingi imesema upande wa kulia ni nzuri zaidi kuliko kushoto. Katika lugha hizi, kulia ina maana ya dini na dhati, na kushoto ina maana ya uovu na jahanamu. Tabia ya lugha hii iko jamii nyingi duniani yote, lakini hasa katika Ulaya na Afrika.

Sina msamiati mpya sana, lakini maneno machache mpya yako hapa:

mageuzi: change
athari: effect
kuzuia: to prevent
kuukilia: to determine
mgusano: contact
kugawanya: to divide
kwa mujibu wa: according to
dhati: sacred
uovu/mwovu: evil
jahanamu: hell

--Petero

Monday, September 12, 2011

Uigiziagi tatu

Katika darasa la Uigizaji tatu tulisomwa michezo ya kirusi mitatu. Mwandishi wa michezo ni Anton Chekov na bwana David Mamet aliyotafsiri katika kiingereza. Wakati watu wanajaribu kufanya mchezo walihitaji kufanya utafiti kuhusu mchezo ule na maisha wa miundo. Bila kazi kabla ya mazoezi itakuwa vigumu kufanya kazi kizuri katika mazoezi.

Chekov aliandishi kuhusu watu tajiri sana katika Urusi. Lakini Ngugi wa Thiong'o ni mwandishi wa Kenya. Yeye ni mtu maalum nchini Kenya. Ngugi aliandishi kuhusu watu wa Kenya na maisha wa wananchi bila kitu sana.

Maneno
kirusi: Russian
miundo: characters
mazoezi: rehearsal (exercises)

Almasi 

Utafiti na wanawake wa Singida

tanzania-political-map.jpg


Niliishi mkoa wa Singida kwa miezi kumi na moja kufanya utafiti kuhusu ujauzito na huduma za afya kwa wanawake wajawazito na pia kwa kujifungua.  Niliwauliza wanawake kuhusu utamaduni wa ujauzito na pia huduma bora zaidi kwa muda wa ujauzito na kujifungua.  Nilikaa mjini Singida na pia nilifanya kazi vijijini.  Nilifanya mahojiano mia na tatu na wanawake, moja na mkunga wa jadi kijijini, na pia na wahudumu wa afya kumi na tisa.  Nilimwuliza mwanamke maswali kama kuhusu historia ya uzazi:  Ulijifungua mara ngapi?  Watoto wangapi walifariki na kwa sababu gani?  Ulijifungua wapi? Nyumbani, hospital, au labda njiani?  Nani alihudhuria kujifungua kwako?  Nani alikusaidia kwa muda wa kujifungua?  Alifanya nini?  Ulipendelea kujifungua hospitalini au nyumbani?  Kwa nini?  Na pia niliuliza maswali kama: Ungependa kuwa na watoto wangapi?  Familia inayokuvutia ina watoto wangapi, kwa nini?  Ni lazima mjamzito aende kupata huduma ya afya mara ngapi?  Huduma za afya kwa wanawake ni muhimu?  Kwa nini ndiyo au hapana?   Nani harusiwi kuwepo wakati wa kujifungua?  Wanawake wajawazito hutendewa tofauti na wanawake wasio wajawazito?  Vipi?

Nilitaka kujifunza kuhusu ujauzito na kuwasikiliza wanawake kwa sababu bado wanafariki kwa muda wa kujifungua au wanajifungua bila msaada wa mkunga.  Naamini kwamba ni haki ya watu wote kuwa na afya kwa muda wa ujauzito na kujifungua.  Kuna shida nyingi unaweza kupata ukiwa na mimba.  Unaweza kupata malaria na ukiwa na malaria ni rahisi zaidi kupata upungufu wa damu.  Upungufu wa damu ni kawaida mkoani Singida.  Kwa muda wa ujauzito ni muhimu sana kula chakula kizuri, bila chakula kizuri kama labda matunda kwa vitamini, na mboga za majani kwa vitamini, mayai, na nyama. Unaweza kupata upungufu wa damu kama huwezi kula nyama na mboga za majani.  Ukiwa na presha ya damu mbaya unaweza kupata kifafa cha mimba na wanawake wanafariki au watoto wanaweza kufariki kwa sababu ya kifafa cha mimba.  Ni muhimu kwenda kliniki kupata huduma kwa muda wa ujauzito kwa sababu utapimwa kwa UKIMWI, upungufu wa damu, malaria, na kwa maambukizo.  Wiki ijayo nitaleta rekodi za mahajiano na wanawake wawili au watatu!    


Msamiati
historia ya uzazi- reproductive history
kujifungua- to give birth
utafiti- research
kituo cha afya- healthcare center
zahanati- dispensary
mahojiano- interviews
wahudumu wa afya- healthcare workers
uzazi wa mpango- family planning
mkunga (wa jadi)- midwife (traditional)
kifafa cha mimba- pregnancy seizures (eclampsia)
upungufu wa damu- anemia

Bi Adriana

Sunday, September 11, 2011

Safari ya Mto de Peres

Kwa darasa ya semina ya mazingira, tulienda sehemu nyingine ya mto de Peres. Mto de Peres una
historia poa sana. Mto uliishi bila shida mpaka mji wa St. Louis ulitaja mahala ya sherehe ya dunia. Watu
wa St. Louis walitambua kwamba mji unanuswa mbaya sana. Kwa hivyo, serikali ilianza kubadilika njia
ya mto. Ilijenga njia chini ya ardhi kwa mto kufuata. Mto ulitiririka chini ya ardhi katika mji wa chuo
kikuu na Forest park. Mto ulipanda juu ya ardhi mashariki ya Forest park. Serikali ulijenga handaki
kuzuia watu kulalamika walipofika sherehe. Haijali kuhusu watu wengine katika St. Louis. Sasa, mto
unaendelea kutiririka chini ya ardhi huko.


Carrie

Wednesday, September 7, 2011

Muziki wa Kiswahili

Angalia vidio hii ya X Plastaz, wanamuziki kutoka Tanzania: http://www.youtube.com/watch?v=UiIa2i29PZ4

Msipofahamu Kiswahili (au Sheng), maneno yako hapa: http://www.myspace.com/xplastaz/blog/420837765

--Bwana Pete