Tuesday, November 8, 2011

Wanawake wanaochagua kujifungua nyumbani

Kwa darasa lingine nafanya utafiti kuhusu uzaliwa nyumbani hapa, mjini St. Louis na pia Marekani kwa jumla.  Nimefanya mahojiano na wanawake waliojifungua nyumbani na pia wahudumu wa afya kama wakunga na "doula".  Sijui kama kuna neno kwa doula kwa Kiswahili lakini doula ni mtu, mwanamke kwa kawaida, anayemsaidia mama kwa muda wa kujifungua.  Anamsaidia mama na mambo mengi kwa mfano, mama akichagua kujifungua kwenye hospitali labda ataandika mipango ya uzaliwa lakini anapoenda hospitalini ni ngumu zaidi kuwaambia wahudumu kusikiliza na kufuata mipango.  Labda mwuguzi atasema mama anahitaji epidural lakini mama ameshaamua kujifungua bila madawa.  Mwuguzi au daktari atajaribu kumwambia mama ni lazima apate epidural kwa sababu ya afya ya mtoto.  Doula atamsaidia mama kusema hapana, anataka kufuata mpango kujifungua bila madawa.  Sasa nimezungumza na wanawake wawili, doula wawili, na mkunga mmoja.  Pia, nimehudhuria mkutano ya "Rafiki wa Wakunga wa Missouri" na tulizungumza kuhusu kujifungua nyumbani na hospitalini.  Ukijifungua nyumbani na msaada ya mkunga unafuata mfano ya ukunga.  Ukunga ni tofauti sana kwa sababu mwanamke anatendewa kama mtu mzima, mwili na ubongo ni kama kitu kimoja, bila mpasuko Cartesian.  Pia, mwanamke na familia yake wanaweza kuamua eneo la uzaliwa na anataka kujifunguaje.  Si kawaida kujifungua nyumbani Marekani, ni kama asilimia mbili au tatu tu lakini kwa maoni yangu wanawake zaidi wanahitaji kujifunza kuhusu uzaliwa nyumbani.

Msamiati
uzaliwa nyumbani- home birth
mkunga- midwife
ukunga- midwifery
mpasuko- split (Cartesian split in this case)
mwuguzi- nurse

Adrienne

No comments:

Post a Comment