Kwa utafiti wangu niliishi kijijini Nkungi kwa muda wa miezi minne. Ningeenda kwa basi kila Jummapili na ningerudi kila Alhamisi. Tulikuwa na shida kubwa sana na umeme kijijini na pia mara kwa mara hatukuwa na maji kwa sababu ya ukosefu wa umeme. Mwezi wa sita nilimsaidia rafiki yangu kuvuna mahindi. Ni kazi ngumu kuvuna. Nilikatwa na mahindi na mwaka huu hatukuwa na mvua ya kutosha kwa hivyo kulikuwa wadudu wengi sana kwenye mahindi. Pia kijijini, nilimsaidia rafiki yangu kusaga mahindi na nilijifunza kupika chakula kitanzania. Nilijifunza kupika na jiko la mkaa. Nilijifunza kupika maandazi, pilau, kuku, chapati, maharage, na makande. Napenda kufanya mazoezi asubuhi kabla ya kufanya kazi ninapoishi kijijini kwa sababu naweza kukimbia bila kusumbuliwa na watu wengine. Kila siku nilienda kijijini kingine kumsaidia mhudumu wa afya. Nilijifunza kuchanja sindano na kuwasaidia mama wajawazito walipokuja kliniki. Niliwahoji mama kila siku pia. Napenda kijiji cha Nkungi sana na sasa nawamisi marafiki yangu kijijini.
Msamiati
kuvuna- to harvest
kuhoji- to interview
makande- rice and corn dish
kusaga- to grind
jiko la mkaa- charcoal stove
kusumbuliwa- to be annoyed
No comments:
Post a Comment