Wednesday, November 30, 2011

Nilipopanda Mlima Kilimanjaro

Mwezi wa saba mwaka huu nilipanda mlima Kilimanjaro na rafiki yangu Ryan.  Tuliamua tulitaka kupanda mlima mwezi wa tatu au mwezi wa nne.  Tulihitaji kufanya mazoezi kabla ya kupanda kwa sababu ni kazi ngumu sana kupanda mlima.  Tilienda mji wa Moshi kwa basi siku moja na tulichagua vitu kutumia kwa muda wa kupanda.  Tulipata vitu kama jaketi kubwa, buti, na mizigo.  Tuliwakutana watu wengine waliotusaidia kupanda kama "camp master", mpishi, na kiongozi wetu.  Tuliamua kupanda kwa njia Machame.  Watu wanasema njia hii ni ngumu lakini unaweza kuona mazingira tofauti tofauti na mazuri sana.  Ni siku sita ukipanda njia Machame.  Siku ya kwanza tulitembea kwenye msitu wa mvua.  Mvua ilinyesha lakini tulikuwa tayeri na hatukuwa na shida yoyote.  Kila siku tulitembea kwa masaa mengi, siku moja masaa sita, siku nyingine masaa manane au zaidi.  Tuliamka na tulianza ketembea.  Ni muhimu sana kula chakula ya kutosha na kunywa maji mengi sana kama lita tano au zaidi.  Watu wengine walikuwa na shida na magonjwa ya mwinuko.  Kwa mfano unaweza kupata shida ya kuhema au unaweza kusikia kizunguzungu au unaweza kutapika.  Sikuwa na shida.  Siku ya kufika kileleni tuliamka saa sita usiku na tulitembea gizani kwa masaa sita.  Baada ya macheo tulitembea kwa masaa matatu kabla ya kufika kilele.  Tulirudi base camp kupumzika kwa muda mfupi alafu tuliendelea kutembea.  Nafikiri tulilala kwa saa moja tu usiku ya kufika kileleni.  Sijawahi kuchoka kama siku hizo.  Nimefurahi sana kufika kileleni!  Unahitaji kuwa na fedha nyingi sana kupanda mlima kama wewe ni mzungu lakini nafikiri kuweza kuona mlima ni ya kufaa.  Sitasahau kupanda Kilimanjaro.

Msamiati
kupanda mlima- to climb a mountain
kilele- summit
ya kufaa- worthwhile
macheo- sunrise
kizunguzungu- dizziness
magonjwa ya mwinuko- altitude sicknesses









Adrienne

No comments:

Post a Comment