Monday, October 3, 2011

Wanawake wajawazito wanatendewa vipi?

Nilipozungumza na wanawake nilimwuliza "Je, wanawake wajawazito hutendewa tofauti na wanawake wasio wajawazito?"  Hapa, Marekani, nafikiri mwanamke mjamzito anatendewa tofauti.  (Sina watoto kwa hiyo sijui kwa kweli lakini naona anatendewa tofauti.)  Kwa mfano, akikaa Marekani, mjamzito anaweza kupumzika zaidi na anaweza kwenda hospitalini kumwona daktari labda mara kumi na mbili au zaidi.  Mume wake anamsaidia na kazi au kufanya mipango kwa kujigungua, kupataje huduma za afya kwa muda wa ujauzito na kadhalika.  Baada ya uzazi wa mtoto mama anaweza kuacha kazi kwa muda wa miezi mitatu na mara kwa mara (sasa ni kawaida zaidi kuliko zamani) baba wa mtoto anaweza kuwa na likizo pia.  Mjamzito anaweza kusoma vitabu vingi sana kuhusu ujauzito na kuhusu huduma za afya kwa muda wa ujauzito na kujifungua na kwa mtoto.

Wajawazito wanaokaa Tanzania hawawezi kufanya mipango kama Wamarekani.  Labda mume wake anamsaidia kupata chakula au majirani au wifi wanamsaidia na kazi ya nyumbani.  Lakini wanawake wengi vijijini waliniambia kwamba hawawezi kuacha kazi na mume hafanyi kitu chochote kwa muda wa kujifungua au kwa muda wa ujauzito.  Ni muhimu sana kutofanya kazi ngumu sana kwa sababu mimba inaweza kuharibika.  Akifanya kazi ngumu kama kuchota maji au kubeba mizigo mjamzito anaweza kupata shida hata shida na mtoto, mtoto anaweza kufariki tumboni.  Baada ya uzazi wa mtoto ni kazi ya wanawake tu.  Labda baba wa mtoto atachinja mbuzi kuadhimisha uzazi lakini hamsaidia mama na mtoto kwa kweli.  Wanawake wanakuja kumsaidia mama mpya, kama mama mzazi, wifi, dada, au majirani.  Unaweza kumkuta wanawake wajawazito ambao wana afya mbaya, labda kwa sababu hawana msaada na kazi au hawawezi kupata lishe bora na ukimwona mama mjamzito na ana afya mbaya labda ni kwa sababu hana mume au ana mume mbaya.

Msamiati
kutendewa- to be treated
wifi- sister-in-law
uzazi- birth
kuchota maji- to fetch water
lishe- nutrition
kuchinja- to slaughter
kuadhimisha- to celebrate

Adrienne

No comments:

Post a Comment