Monday, September 19, 2011

Wanawake na huduma za afya Tanzania


Kuna tofauti nyingi sana na huduma za afya za Tanzania na huduma za afya za Marekani.  Majengo ni tofauti sana.  Marekani unaenda hospitali na unaingia jengo moja kwa kawaida lakini hospitali za Tanzania ziko nje.  Unatembea nje unapoenda wodini.  Wanawake wanasubiri nje wanapokuja kujifungua pia.  Hawana vifaa na mara kwa mara hukuna wahudumu wa afya au wahudumu hawana elimu bora.  Nasikitika ninapoona zahanati za Tanzania na ninapowaona wanawake wanatendewa vipi wanapoenda kupata huduma za afya kwa muda wa ujauzito au kujifungua.  Kwa mfaano, niliangalia manasi waliompiga mwanamke kwa sababu alipiga kelele alipokuwa na uchungu na aliposukuma kwa muda wa kujifungua.  Wahudumu wachache wanafikiri kwamba wanawake wanaotoka shambani hawana elimu na wao ni wajinga na wahudumu wanawaonea wanawake.

Msamiati
-onea: look down on someone
wodi- medical ward
shamba-field
uchungu- contractions/ labor pains
vifaa- tools/equipment

No comments:

Post a Comment