Monday, September 26, 2011

Uzazi wa mpango na ukubwa wa familia



Bado watu wa Tanzania wanataka kuwa na watoto wengi sana.  Ni kawaida nchini kuwa na watoto watano au zaidi.  Watu wa masikini wana watoto wengi lakini na watoto wengi hawataweza kulipia shule na watoto watamaliza na darasa la saba na hawataweza kuendelea na masomo.  Ni mbaya sana hasa kwa wanawake.  Kama familia ina watoto watano, wawili wakiume na watatu wakike, ni kawaida zaidi kwamba watoto wakiume wataweza kuendelea na shule baada ya shule ya msingi.  Wasichana watakaa nyumbani mpaka wamemtafuta mume.  Familia nyingi sana haitumii uzazi wa mpango kwa sababu mama hawezi kwenda kliniki kila mwezi au labda baba hamtaki mke wake kutumia dawa za kukinga ujauzito.  Nilimwona mama mmoja aliyekuwa na miaka hamsini na tatu na alikwepo hospitalini kujifungua mtoto wa kumi na moja au kumi na mbili.  Amechoka sana na hawezi kuwa na maisha kwa kweli.  Bila shaka mama huu ana binti ambaye ana mtoto pia.  Ni muhimu sana kwa afya ya mama na afya na watoto wote wa familia kutumia uzazi wa mpango.

Pia, nafikiri ni muhimu sana kuwafundisha wanafunzi wa shule ya sekondari kuhusu uzazi wa mpango, kwa mfaano kutumiaje kondom au dawa ya kukinga ujauzito.  Hawajui na wasichana wanapata mimba. Hairusiwi kuhudhuria shule ukiwa na mimba.  Wanahitaji kutoka shule.  Labda wanaweza kurudi shuleni baada ya kujifungua lakini si kawaida.  Pia, ni ya hatari kupata mimba akiwa na miaka kumi na tano, kumi na sita kwa sababu hajamaliza kukua, labda atapata shida na nyonga na atahitaji upasuaji.

Msamiati
uzazi wa mpango- family planning
mimba- pregnancy
dawa ya kukinga ujauzito- medicine to prevent pregnancy (the pill, etc.)
Hairusiwi- it's not allowed
-a hatari- dangerous
kukua- to grow 
nyonga- hip/s

Adrienne

No comments:

Post a Comment