Wednesday, November 2, 2011

Muziki ya Bongo Flava

Kuna aina ya muziki katika Afrika Mashariki, hasa mijini Nairobi na Dar es Salaam, inayeitwa "Bongo Flava." Aina hii inatoka muziki ya hip hop ya Amerika, na R&B, na Taraab kutoka pwani ya Kenya, na aina za muziki kienyeji katika Tanzania. Mara kwa mara Bongo Flava inatumia ushairi wa Kiswahili kuumba maneno yao.

Na pia, Taraab na aina zingine za muziki wa ng'ambo zimepa Bongo Flava matumizi ya ghani, ambazo ni toni za lugha za Bantu hazizohudhuria katika Kiswahili. Wanamuziki wa Bongo Flava husema kwamba ghani hizi zinapa muziki tabia za "Blues", kama katika Amerika. Wanamuziki wanapoimba, wanatumia Kiswahili na Kiingereza na lugha zingine za Afrika. Kwa hivyo, Bongo Flava ni mchanganyiko wa aina nyingi za muziki kutoka pahali pengi duniani yote. Sasa, redio ya Bongo Flava nzuri zaidi iko mjini Chicago, kwa hivyo muziki hii imeenea duniani yote.

Muziki hii inazungumza kuhusu swala nyingi katika jamii za Waafrika, hasa njia kwa watu kuziboresha maisha zao. Kwa hivyo, maneno ya wimbo hizi yanamudu na ukimwi na ndoa, na pesa na kadhalika. Ingawa hip hip ya Amerika mara kwa mara ni dhalimu na mkali, hip hop ya Tanzania ina furaha zaidi, na wamuziki hawa wanajaribu kutumia muziki yao kujaza moyo na kuboresha maisha za watu katika jamii zao. Kwa sababu ya utofauti hii, wanamuziki wa Bongo Flava husema kwamba muziki zao ina tofauti na hip hop, hasa hip hop ya Amerika.

http://www.youtube.com/watch?v=uAU1QQtn7EE

http://www.youtube.com/watch?v=atsGXqwtG5s

Msamiati:
kuenea - to spread outwards
kuhudhuria - to be present
ghani - tones (in language)
dhalimu - violent

--Pete

No comments:

Post a Comment