Wednesday, November 16, 2011

Ebrahim Hussein

Bwana Hussein, mwandishi wa "Wakati Ukuta," tamthilia yetu, ni mwandishi wa Tanzania maalum zaidi. Anatoka familia ya Waarabu, na amekitumia Kiswahili kuandika tamthilia zake zote, na hajazitafsiri hadi Kiingereza au lugha nyingine.

Katika Kenya, kumekuwa na waandishi Wakenya wengi wameoandika tamthilia zao kwa Kiingereza badala ya Kiswahili kwa sababu ya urahisi ya Kiingereza kuenea n'gambo na kusomwa na Walaya au Wamerika, lakini hakujakuwa na waandishi Watanzania wameoandika tamthilia zao kwa Kiingereza--kwa Kiswahili tu. Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa lugha ya taifa katika Tanzania, na Ujamaa iliwasababisha waandishi wengi kutumia Kiswahili, ingawa kisha zingekuwa ngumu zaidi kuzichapisha n'gambo.

Kwa hivyo, tamthilia za Bwana Hussein hazijasomwa nyingi nje ya Tanzania na Kenya, lakini anajuliwa kama mwandishi wa Tanzania mzuri zaidi, hasa leo. Tamthilia zake nyingi zinahusika Ujamaa na jamii za Tanzania, lakini kwa sababu ya ugumu ya kuandika kwake, watu wengi hawawezi kumsoma na kumfahamu. Kiswahili chake ni kigumu zaidi kwa watu wengi sana, na kwa hivyo watu wengi wanadhani vitu vibaya kuhusu yeye na kuandika kwake.

Watu wachache wasema kwamba hajui kuhusu "ujamaa" na maswali ya watu wa kawaida. Lakini pia watu wa nje ya Afrika Mashariki hawawezi kusoma tamthilia zake pia kwa sababu ya maswala ya lugha, na kwa hivyo yeye hajasomwa kila mahali duniani bado.

--Pete

Msamiati mpya (labda):

maalum - famous, important
kuchapisha - to publish
kuhusika - to concern, deal with
ugumu - difficulty

No comments:

Post a Comment