Wednesday, November 30, 2011

Kaka yangu

Mchumba wa kaka yangu ana mimba. Nilifunza majira ya joto iliyopita, wakati kakangu aliita mimi na simu na alisema "Melissa ana mimba." Nilisema "Kweli" basi alisema "Hapana."

Wazazi zetu walishtuka sana lakini sasa familia yangu inapa msaada sana. Mchumba wa kakangu pia alisema kwa kwanza wazazi wake walikuwa na hasira kwa sababu wazazi ni watu wakristo sana.

Wakati shukrani, kakangu na mchumba walikaa nyuba yetu kwa wiki hii. Niliona kwamba kakangu alikomaa sana sasa; alitaka kujaribu kuanzisha kampuni.



msamiati
mchumba - girlfriend
mimba -pregnant
kukomaa - mature
kampuni - company
wakristo - christian


-pat

Mapokeo ya Kiswahili

Kuna mapokeo katika tamaduni zote duniani. Wiki hii, Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, alivunja mwiko alipomwoa mke wake katika Novemba, imeyeharimishwa katika utamaduni ule.

Katika tamaduni za Afrika Mashariki, hasa utamaduni wa Waswahili, kuna desturi ndefu sana ya mapokeo haya, na aina moja kuonya shagala kama hizi ni kuenea methali dhidi ya zile. Hapa ziko methali chache za Kiswahili zinazowaonya watu dhidi ya mapokeo fulani:

Kukutana na paka mweusi usiku ni nuksi.

Kula gizani ni kula na shetani.

Kuuza chumvi usiku ni nuksi kwa mwenye duka.

Mtu akila bila ya kupiga Bismillahi, basi baraka itaondoka na mtu hataweza kushiba.

Kuzaliwa na vidole sita ni mabruki.

Kutembea hali ya kuwa amevaa kiatu kimoja tu kunavimbisha ziwa la mama yake mtu.

Msamiati (mpya):
kuvunja mwiko - to break a taboo
kuharimisha - to make a taboo
pokeo/ma-  - superstition
kuonya - to warn against...
shagala - activity
kuenea - to spread
desturi - tradition
dhidi ya - against...
nuksi - bad luck/omen
mabruki - blessing
kuvimba - to swell

--Petero

Alberici

Jana, nilienda Alberici na darasa la mazingira.  Alberici ni kampuni ya ujenzi ambaye inajenga majengo mazuri kwa mazingira. Alberici ilikuwa ujenzi kwa miaka mengi sana, lakini karibuni ilibadili kujenga majengo ambayo ni "LEED".  LEED inabainisha maongozi kwa kujenga majengo yana athari ndogo juu mazingira.  Viwango cha LEED ni silver, dhahabu, na platinamu.

Alberici ilijenga Brauer Hall kwa Wash U, jengo la mahandisi jipya.  Brauer ilipokea cheo cha dhahabu.  
Brauer ilijengwa na vifaa vinatumiwa tena. Pia, vifaa vingi vinakuja ndani mia tano miles.  Brauer ilijengwa kutumia nafasi ndogo na kuongeza nafasi kwa kupanda mmea.  Pia, chini ya ardhi, kuna "cistern"ambaye inakamata maji wa mvua na maji inatumia tena kwa azimio nyingine.


ujenzi: construction
maongozi: guidelines
kubainisha: to specify
athari: impact
viwango: levels/statuses
mhandisi: engineer
cheo: rank, status
dhahabu: gold
vifaa: materials
mmea: plant
kukamata: detain, catch
azimio: aim

Wasaani- Almasi

Nilipokuwa na Kenya, nilikuwa na wasaani kwa masaa mengi kwa mwezi wa mwisho. Wasaani wanapenda kuvuta sigara sana. Kila kitu ambacho nilikutana walipenda kuvuta sigara. Pia, walipenda kuimba ‘kareoke’ pamoja. Kila jumatano baada ya kazi tulienda disco kuimba ‘kareoke’ na kunywa Tusker. Baada ya disco tulienda ‘Ken-chick’, pale tulikula kuku katika karatasi ya shajara.

Kenya ni nchi ndogo, kwa hivyo wasaani walijuana. Yaani, rafiki yangu alinijulisha mtu anaitwa Moses. Moses ni mtu ambaye ni bora ya pili mwanamuziki wa keyboard katika Kenya. Nilipomkutana anliniuliza kuimba siku moja naye na bendi yake. Sikufikri ni kweli. Lakini siku ya chache baadaye rafiki yangu na mimi tulienda mkahawa wapi Moses alicheza. Waliniuliza tena kuimbi, nilishtua, lakini ‘ndiyo’ na nilichagua  kuimba ‘Watu wa kawaida’. Nilisahau maneo chache lakini ninafikiri wimbo ambao niliimbi ulikuwa nzri. Sikia!   


Wasaani: Artists/performers
Shajara: notebook
-julisha: introduce   
mwanamuziki: musician
bendi: band

Nilipopanda Mlima Kilimanjaro

Mwezi wa saba mwaka huu nilipanda mlima Kilimanjaro na rafiki yangu Ryan.  Tuliamua tulitaka kupanda mlima mwezi wa tatu au mwezi wa nne.  Tulihitaji kufanya mazoezi kabla ya kupanda kwa sababu ni kazi ngumu sana kupanda mlima.  Tilienda mji wa Moshi kwa basi siku moja na tulichagua vitu kutumia kwa muda wa kupanda.  Tulipata vitu kama jaketi kubwa, buti, na mizigo.  Tuliwakutana watu wengine waliotusaidia kupanda kama "camp master", mpishi, na kiongozi wetu.  Tuliamua kupanda kwa njia Machame.  Watu wanasema njia hii ni ngumu lakini unaweza kuona mazingira tofauti tofauti na mazuri sana.  Ni siku sita ukipanda njia Machame.  Siku ya kwanza tulitembea kwenye msitu wa mvua.  Mvua ilinyesha lakini tulikuwa tayeri na hatukuwa na shida yoyote.  Kila siku tulitembea kwa masaa mengi, siku moja masaa sita, siku nyingine masaa manane au zaidi.  Tuliamka na tulianza ketembea.  Ni muhimu sana kula chakula ya kutosha na kunywa maji mengi sana kama lita tano au zaidi.  Watu wengine walikuwa na shida na magonjwa ya mwinuko.  Kwa mfano unaweza kupata shida ya kuhema au unaweza kusikia kizunguzungu au unaweza kutapika.  Sikuwa na shida.  Siku ya kufika kileleni tuliamka saa sita usiku na tulitembea gizani kwa masaa sita.  Baada ya macheo tulitembea kwa masaa matatu kabla ya kufika kilele.  Tulirudi base camp kupumzika kwa muda mfupi alafu tuliendelea kutembea.  Nafikiri tulilala kwa saa moja tu usiku ya kufika kileleni.  Sijawahi kuchoka kama siku hizo.  Nimefurahi sana kufika kileleni!  Unahitaji kuwa na fedha nyingi sana kupanda mlima kama wewe ni mzungu lakini nafikiri kuweza kuona mlima ni ya kufaa.  Sitasahau kupanda Kilimanjaro.

Msamiati
kupanda mlima- to climb a mountain
kilele- summit
ya kufaa- worthwhile
macheo- sunrise
kizunguzungu- dizziness
magonjwa ya mwinuko- altitude sicknesses









Adrienne

Wednesday, November 16, 2011

Ebrahim Hussein

Bwana Hussein, mwandishi wa "Wakati Ukuta," tamthilia yetu, ni mwandishi wa Tanzania maalum zaidi. Anatoka familia ya Waarabu, na amekitumia Kiswahili kuandika tamthilia zake zote, na hajazitafsiri hadi Kiingereza au lugha nyingine.

Katika Kenya, kumekuwa na waandishi Wakenya wengi wameoandika tamthilia zao kwa Kiingereza badala ya Kiswahili kwa sababu ya urahisi ya Kiingereza kuenea n'gambo na kusomwa na Walaya au Wamerika, lakini hakujakuwa na waandishi Watanzania wameoandika tamthilia zao kwa Kiingereza--kwa Kiswahili tu. Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa lugha ya taifa katika Tanzania, na Ujamaa iliwasababisha waandishi wengi kutumia Kiswahili, ingawa kisha zingekuwa ngumu zaidi kuzichapisha n'gambo.

Kwa hivyo, tamthilia za Bwana Hussein hazijasomwa nyingi nje ya Tanzania na Kenya, lakini anajuliwa kama mwandishi wa Tanzania mzuri zaidi, hasa leo. Tamthilia zake nyingi zinahusika Ujamaa na jamii za Tanzania, lakini kwa sababu ya ugumu ya kuandika kwake, watu wengi hawawezi kumsoma na kumfahamu. Kiswahili chake ni kigumu zaidi kwa watu wengi sana, na kwa hivyo watu wengi wanadhani vitu vibaya kuhusu yeye na kuandika kwake.

Watu wachache wasema kwamba hajui kuhusu "ujamaa" na maswali ya watu wa kawaida. Lakini pia watu wa nje ya Afrika Mashariki hawawezi kusoma tamthilia zake pia kwa sababu ya maswala ya lugha, na kwa hivyo yeye hajasomwa kila mahali duniani bado.

--Pete

Msamiati mpya (labda):

maalum - famous, important
kuchapisha - to publish
kuhusika - to concern, deal with
ugumu - difficulty
Sasa, katika Tisch Commons katika DUC, kuna mhadhara na Kate Geagan. Kate Geagan ni "nutritionist" au "dietician," mtu ambaye anafunza watu kuhusu chakula ungekula kunawiri.  Lakini, yeye ni tofauti ya "nutritionist" nyingine kwa sababu yeye anafikiri chakula ambacho kinasaidia mazingira ni muhimu sana.  Kate Geagan anaeleza vipi kula chakula kizuri na kusaidia mazingira.  Kwa mfano, anapendekeza  watu wanakula mboga na maharagwe mengi kila mlo.  Samaki, kuku, na nyama ingekuliwa mara chache tu.  Nyama inatumia kawi kuliko ya mboga kuauni mtu na kawi sawa ya nyama kama ng'ombe.

Pia, Kate anazungumza kuhusu kula chakula na azimio kufika lengo la uzito.  Anaeleza kwamba watu wanahitaji kula kulisha mwili, si kufurahia tu.  Ukitaka, Kate anakupewa "menu" ya chakula kizuri kula kwa wiki moja kujaribu maisha mapema.



mhadhara = lecture
kunawiri = to be healthy
kupendekeza= to recommend
mboga = vegetables
maharagwe= beans
mara chache = rarely
mlo = meal/fare
kuauni = provide
azimio = goal, intention
lengo = goal
mwili = body