Tuesday, October 18, 2011

Harusi ya rafiki yangu

Nilipokuwepo Tanzania mpanzi wangu na mimi tulihudhuria harusi ya rafiki yangu.  Rafiki yangu anaitwa Tom na mke wake anaitwa Rafia au Catrina.  Catrina ni jina lake la kikristo.  Alizaliwa Mwislamu lakini Tom ni Mkristo na Rafia alitanasari baada ya uzaliwa wa mtoto wao.  Siku moja kabla ya harusi tulienda nyumbani ya wazazi wa Tom na watu wote wa familia ya Tom na familia ya Rafia walienda kula chakula cha jioni pamoja.  Siku ya harusi tulienda nyumbani ya familia ya Tom kwanza kupiga picha.  Alafu, tuliendelea na familia yoyote kanisani.  Familia ya Rafia haikuenda kanisani.  Baada ya kanisa tulirudi nyumbani ya wazazi wa Tom kupumzika kidogo na kunywa maji na soda.  Alafu tulienda hotelini ya kisasa na safi sana kupiga picha ya watu wote.  Baada ya hoteli watu wote walienda ukumbi kula chakula na kusherehekea.  Tulikula chakula kingi sana na tulicheza dansi.  Bwana na bibi harusi walipendeza sana.

Msamiati
-tanasari- to convert from Islam to Christianity
-sherehekea- to celebrate
bwana harusi- groom
bibi harusi- bride
Bwana na bibi harusi

Rafiki yangu Tom na kakake wawili (Edward na David) na dadake mmoja (Diana).

Bwana na bibi harusi na keki
Adrienne

No comments:

Post a Comment