Monday, September 12, 2011

Utafiti na wanawake wa Singida

tanzania-political-map.jpg


Niliishi mkoa wa Singida kwa miezi kumi na moja kufanya utafiti kuhusu ujauzito na huduma za afya kwa wanawake wajawazito na pia kwa kujifungua.  Niliwauliza wanawake kuhusu utamaduni wa ujauzito na pia huduma bora zaidi kwa muda wa ujauzito na kujifungua.  Nilikaa mjini Singida na pia nilifanya kazi vijijini.  Nilifanya mahojiano mia na tatu na wanawake, moja na mkunga wa jadi kijijini, na pia na wahudumu wa afya kumi na tisa.  Nilimwuliza mwanamke maswali kama kuhusu historia ya uzazi:  Ulijifungua mara ngapi?  Watoto wangapi walifariki na kwa sababu gani?  Ulijifungua wapi? Nyumbani, hospital, au labda njiani?  Nani alihudhuria kujifungua kwako?  Nani alikusaidia kwa muda wa kujifungua?  Alifanya nini?  Ulipendelea kujifungua hospitalini au nyumbani?  Kwa nini?  Na pia niliuliza maswali kama: Ungependa kuwa na watoto wangapi?  Familia inayokuvutia ina watoto wangapi, kwa nini?  Ni lazima mjamzito aende kupata huduma ya afya mara ngapi?  Huduma za afya kwa wanawake ni muhimu?  Kwa nini ndiyo au hapana?   Nani harusiwi kuwepo wakati wa kujifungua?  Wanawake wajawazito hutendewa tofauti na wanawake wasio wajawazito?  Vipi?

Nilitaka kujifunza kuhusu ujauzito na kuwasikiliza wanawake kwa sababu bado wanafariki kwa muda wa kujifungua au wanajifungua bila msaada wa mkunga.  Naamini kwamba ni haki ya watu wote kuwa na afya kwa muda wa ujauzito na kujifungua.  Kuna shida nyingi unaweza kupata ukiwa na mimba.  Unaweza kupata malaria na ukiwa na malaria ni rahisi zaidi kupata upungufu wa damu.  Upungufu wa damu ni kawaida mkoani Singida.  Kwa muda wa ujauzito ni muhimu sana kula chakula kizuri, bila chakula kizuri kama labda matunda kwa vitamini, na mboga za majani kwa vitamini, mayai, na nyama. Unaweza kupata upungufu wa damu kama huwezi kula nyama na mboga za majani.  Ukiwa na presha ya damu mbaya unaweza kupata kifafa cha mimba na wanawake wanafariki au watoto wanaweza kufariki kwa sababu ya kifafa cha mimba.  Ni muhimu kwenda kliniki kupata huduma kwa muda wa ujauzito kwa sababu utapimwa kwa UKIMWI, upungufu wa damu, malaria, na kwa maambukizo.  Wiki ijayo nitaleta rekodi za mahajiano na wanawake wawili au watatu!    


Msamiati
historia ya uzazi- reproductive history
kujifungua- to give birth
utafiti- research
kituo cha afya- healthcare center
zahanati- dispensary
mahojiano- interviews
wahudumu wa afya- healthcare workers
uzazi wa mpango- family planning
mkunga (wa jadi)- midwife (traditional)
kifafa cha mimba- pregnancy seizures (eclampsia)
upungufu wa damu- anemia

Bi Adriana

No comments:

Post a Comment