Wednesday, September 28, 2011

Mashairi ya Kiswahili

Kumekuwa na wendo wa ushairi wa Kiswahili, kutoka mashairi ya kale mpaka mashairi ya kisasa--kuna utofauti za lugha, na mita, na aina zingine. Wendo hizi umeruhusu watu wengi kutumia ushairi, watu wachache katika Mombasa na pwani ya Kenya wanafikiri mashairi ya kisasa yana tatizo kasoro kuliko aina za kale. 

http://www.youtube.com/watch?v=N0t7WQbnzZg&feature=related

Vidio hii ni ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Indiana, akikariri shairi la kale la Shabaan Bin Robert, linaloitwa "Titi la Mama."


"Titi la Mama," by Shabaan bin Robert

Titi la mama litamu, hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu, sifayo iliyofumbwa,
Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama mlizamu, funika palipozibwa,
Titile mama litamu, Jingine halishi hamu.   

Lugha yangu ya utoto, hata sasa nimekua,
Tangu ulimi mzito, sasa kusema najua,
Ni sawa na manukato, moyoni mwangu na pua,
Pori bahari na mto, napita nikitumia,
Titile mama litamu, jingine halishi hamu.


Na pia, vidio hii ni mfano wa shairi la kisasa la Mrisho Mpoto, kama "Slam Poetry:" 
http://www.youtube.com/watch?v=9ypibltbjb8


Msamiati:


msomi - scholar
kuunda - to create
kukariri - to recite
fumbo - riddle
kufifia - to decline, die off
wendo - movement, process
kuruhusu - to allow
kutii - to conform, obey
tatizo - complexity

--Petero

No comments:

Post a Comment